DigitalCity(AM3)
DigitalCity Services Limited
2.05.01.17.270688 Varies with device
Sasa kila raia, biashara na kila mali isiyohamishika kwenye nchi za Afrika Mashariki imepata anuani ya kudumu. Ardhi yote ya Afrika Mashariki tumeigawanya kwenye miraba ya ukubwa wa mita tatu kwa tatu (3m x 3m) na kila mraba umepewa anuani maneno matatu. Maneno matatu haya hayana maana yoyote. Ni maneno matatu tu. Ni rahisi kuyakumbuka na ni rahisi kutumia. Ni sawa na majina yako matatu.


Kampuni ya DigitalCity Services Ltd ya Tanzania imeshirikiana na Kampuni ya What3words ya Uingereza kukamilisha mradi huu. Anuani hizi ni maalumu kwa nchi za Afrika Mashariki - Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Democratic Republic of Congo (DRC), Zambia, Southern Sudan and Malawi.


Anuani Maneno Matatu – AM3 inakuwezesha kutambua mahali ulipo, biashara yako ilipo na mahali mali yako ilipo, na unaisajili kwenye rejista ya kudumu ya anuani. Kwa kutumia anuani maneno matatu unaweza kutangaza biashara yako na/au kutafuta bidhaa unayoihitaji iko wapi. Pia unaweza kutafuta anuani za jamaa na marafiki zako na za washirika wako wa biashara na kuwatembelea. Fika mahali unapotaka, wakati wowote na bila kuuliza. Nenda na AM3.

Content rating: Everyone

Requires OS: 4.0.3 and up

...more ...less